Vuka ngambo ya jaribu

 Jivushe ngambo ya jaribu ngaombo ya mapito mbali mbali unayo pitia katika maisha ya kila siku.  siku za utoto wangu nilifikiri kama niliye ishi katika maisha duni sana, hasa hali sa wazazi wangu kiuchumi silinishuhudia bayana kuwa nimtoto dhaifu zana hata kwenye makundi ya watoto niliyo cheza nao.


hali hii ilinisumbua sana akili yangu, na kadri nlivyo endelea kukua niliwaza nakupanga kwamba nilitakiwa nijikimu kiuchumi mapema ili maisha yangu yapate furaha.


na baadae nilipo pata umri wakujihimiza kujikimu kifedha, nilifanya hivyo, kama kijina mbio yangu ilikuwa kubwa sana japokuwa ufanisi sikuupata kama nilivyo weza kupanga,


katika mapito yangu tafuta uchumi epuka umasikini, nikajifunza mambo mengi sana dunia, wazazi wangu walinilea mtoto wakawaida kiimani na kiitikadi kwamaana mbali mbali kwamba sikufunzwa kuwa na imani madubuti wala mkakati endelevu katika maisha ama elimu, nililelewa nikakua nikakutana na ugumu wa maisha.


mapito ya uchumi yakaanza kuwa mwalimu wangu, na sikuwa na namna nikajiunga rasmi na elimu ya ufahamu katika mapito niliyo pitia, nilikuwa mwanafunzi na mwalimu, nikisoma na kujisahihisha nikijipima kama kunasehemu natoka na kuona pahala napo elekea.


miaka ikaenda, elimu ikakua, hali yakuendelea kujifunza katika mapito ikaendelea kunishuhudia kuwa, nikama kwanza ndio nimezaliwa katika kujua hali ya nyakati katika ulimwengu, maana yake ndio kwanza naanza kusoma elimu ya wenyeji wa mwanadamu katika ulimwengu.


tafsiri rahisi ilinilasimu kusoma matendo ya mwanadamu dhidi ya mwanadamu mwingine katika uso wa dunia, nikasoma mengi sana, jumla ya matendo ya mwanadamu duniani ni vitu vyaaibu sana, nilipo jua jambo hili nilihusunika nakukata tamaa, kisha nikajiambia basi mimi nitajiri nisie jifahamu.


kutokea hapa nikawajifunza wale ndugu wautoto, napo nikabaini kiroho wanamaisha ya kutisha na yamatezo makali, ndipo hapo nikajiambia tena, kumbe mimi ni mtu tajiri ila utajiri wangu umefichwa, basi nikapunguza huzuni nahapa, narudi tena darasana, nakama nikafaulu vyema nitarejea na kuwajuza kile nilicho jifunza darasanai. furahia siku yako.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii